Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Amos Makalla Jijini Mwanza alipofika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kabla ya kuanza ziara katika miradi mbalimbali ya Elimu na kufungua Mafunzo ya Maafisa Elimu Kata zaidi ya 600 kutoka Mikoa saba nchini.
Katika Ziara hiyo Mhe. Mkenda atatembelea mradi wa Ujenzi katika Kampasi ya DIT Mwanza, atakagua eneo la Ujenzi wa Chuo cha VETA cha Wilaya ya Sengerema na eneo la Ujenzi wa Kampasi ya Chuo Kikuu Ardhi inatakayojengwa Wilayaji humo.