Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda ameupongeza uongozi wa Shule ya Sekondari ya Uru kwa kuendelea kufanya vizuri katika mitihani ya Taifa.

Pongezi hizo amezitoa Agosti 26, 2024 Mkoani Kilimanjaro akizungumza katika hafla ya Maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa shule hiyo inayomilikiwa na Kanisa Katoliki

Prof. Mkenda amesema kuwa kufanya vizuri kwa shule hiyo ni kutokana na jitihada za walimu na wanafunzi pamoja na ushirikiano mzuri uliopo kati ya shule na wazazi.

"Kanisa Katoliki limekuwa na mchango mkubwa katika elimu, tunaona jinsi linavyoendelea kujenga Shule nchini, kwa niaba ya serikali tunawashukuru sana" ameongeza Prof. Mkenda.Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda ameupongeza uongozi wa Shule ya Sekondari ya Uru kwa kuendelea kufanya vizuri katika mitihani ya Taifa.

Pongezi hizo amezitoa Agosti 26, 2024 Mkoani Kilimanjaro akizungumza katika hafla ya Maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa shule hiyo inayomilikiwa na Kanisa Katoliki

Prof. Mkenda amesema kuwa kufanya vizuri kwa shule hiyo ni kutokana na jitihada za walimu na wanafunzi pamoja na ushirikiano mzuri uliopo kati ya shule na wazazi.

"Kanisa Katoliki limekuwa na mchango mkubwa katika elimu, tunaona jinsi linavyoendelea kujenga Shule nchini, kwa niaba ya serikali tunawashukuru sana" ameongeza Prof. Mkenda.