WAZIRI MKENDA AFANYA ZIARA SEKONDARI YA WAMA SHARAF
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amefanya ziara latika Shule ya Sekondari ya Wama Sharaf iliyopo mkoani Lindi kujionea hali ya utoaji elimu shuleni hapo.
Akiwa shule hapo waziri mkenda amewaasa wanafunzi kusoma kwa bidi kuwa na maadili kwani ndio msingi wa mafanikio.
"Mafanikio yanaanza na nidhamu, niwaombe tudumishe nidhamu, tusome kwa bidii ili kufikia malengo mliyojiwekea," amesema Prof Mkenda
Waziri Mkenda ameipongeza Taasisi ya WAMA kwa kuwezesha watoto wa kitanzania ambao pengine wasingeweza kusoma kutokana na changamoto za kimazingira kupata elimu na kwamba Serikali itashirikiana nao kuhakikisha watoto hao wanapata elimu bora.