Kongamano la kwanza lenye dhamira ya kujadili maendeleo ya sasa katika Sayansi, Teknolojia Uvumbuzi yanavyoweza kuchangia maendeleo endelevu katika viwanda na jamii.
‘Vyuo vikuu vimefanya kazi ya kufanya tafiti na kutangaza matokeo ya tafiti hizo yanayosaidia katika usuluhisho wa changamoto za kijamii.’ Amesema hayo Naibu katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Franklin Rwezimula akifungua kongamano hilo.
Aidha, Kwenye Sayansi, Ubunifu na Teknolojia kuna mambo mapya yanayotokea, Chuo Kikuu Cha Dodoma hakipo nyuma kuendana na mabadiliko hayo kupitia tafiti wanazozifanya
Dkt Rwezimula ameongezea kuws tafiti hizo zinazofanywa na Chuo Kikuu cha Dodoma zimekuwa msaada kwa serikali katika kupata majawabu ambayo yanarahisisha ufanyaji wa kazi.
" nimefika leo kuangalia wanachokifanya, wana maonyesho mazuri, kuna teknolojia wamebuni wanafunzi na mpango wao ifikapo mwaka 2026 kiwe ni chuo namba 1 Tanzania ambacho kitakuwa kimetoa machapisho mengi ya matokeo ya tafiti," amesema Dkt. Rwezimula.
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Profesa Lughano Kusiluka amesema kongamano hilo ni la kwanza kwa ajili ya kujadili mambo ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu na limehudhuriwa na wanasayansi wabunifu kutoka ndani na nje ya nchi.
Prof. Kusiluka amesema Chuo Kikuu cha Dodoma kina wataalamu katika idara tofauti ikiwemo mambo ya mabadiliko ya tabia jiografia pamoja na kitengo kinachofundisha namna ya kupambana na majanga na wahandisi wa mambo ya mazingira.