Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Daniel Mushi, amesema Serikali inathamini mchango mkubwa wa wanasayansi, wahandisi, watafiti na wabunifu katika kufikia azma ya kuwa nchi ya uchumi wa viwanda.



Prof. Mushi ametoa kauli hiyo leo Disemba 06, 2024 jijini Dar es Salaam akihutubia katika mahafali ya 18 ya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) ambapo amewasisitiza Wahitimu kutumia kikamilifu elimu waliyoipata kwa maendeleo yao binafsi na taifa kwa ujumla.



Ameeleza kuwa Serikali imeendelea kuongeza fursa za mafunzo na kwamba katika mwaka wa fedha 2023/2024, iliongeza udahili katika Vyuo vya Elimu ya Ufundi kutoka wanafunzi 171,581 hadi wanafunzi 235,804 pamoja na kuendelea kutoa mafunzo kwa wakufunzi kuwajengea uwezo wa ufundishaji wa mitaala inayoendana na mabadiliko ya teknolojia na mahitaji ya soko la ajira