1.0       Utangulizi

Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia imekuwa ikitekeleza Mpango wa kuimarisha Elimumsingi na Sekondari katika Nyanja zote ikiwamo kuinua taaluma kwa kuwa na shule bora za Awali, Awali na Msingi, Sekondari na vyuo vya Ualimu. 

2.0       MAJUKUMU YA SEHEMU YA ITHIBATI YA SHULE

Ili kutekeleza azma hiyo, ofisi ya Kamishna wa Elimu, Idara ya Elimumsingi kupitia Sehemu ya Ithibati ya Shule imekuwa ikitekeleza majukumu mabalimbali likiwamo kusajili shule zote zilizokidhi vigezo. Sambamba na jukumu hilo, majukumu mengine kwa mjibu wa Muundo wa Wizara wa mwaka 2018 ni: 

  1. a. Kuandaa nyaraka na miongozo mbalimbali yenye kuweka viwango vya ubora vya chini vya usajili wa shule;
  2. b. Kuwa chanzo cha kufanyika kwa ukaguzi wa kuchunguza ili kuona kama shule na vyuo vya ualimu vinavyoombewa usajili zimekidhi vigezo;
  3. c. Kuchambua maombi ya usajili wa shule
  4. d. Kuandaa na kutoa vyeti vya usajili wa shule zote zisizo za Serikali zilizokidhi vigezo na kupewa usajili;
  5. e. Kuandaa na kutoa leseni kwa walimu wa kigeni na raia wasio walimu;
  6. f.  Kutunza na kuhuisha taarifa za shule na vyuo vya ualimu vilivyosajiliwa katika kitabu cha usajili;
  7. g. Kufuta usajili wa shule ambazo zimekiuka taratibu za usajili wa shule.
  8. h. Kuandaaa taarifa za robo, nusu na mwaka na kuziwasilisha kwaKamishna wa Elimu.

MFUMO WA USAJILI WA SHULE

FANI 9 ZA ELIMU YA AMALI