KAZI ZA KITENGO
Kitengo cha Mawasiliano serikalini kina jukumu la kutoa utaalamu na huduma katika masuala ya Mawasiliano na Habari kwa Wizara.
Ni kitengo cha kimkakati kinachosaidia utekelezaji wa malengo ya Wizara kupitia Habari, Elimu na Mawasiliano. Hii inahusisha usambazaji wa habari za wizara kwa wakati, kupokea mrejesho na maoni kutoka kwa wadau 
 

MAJUKUMU YA KITENGO

  • Kuzalisha na kusambaza machapisho, nyaraka, makala, vibango ili kuufaamisha umma juu ya sera, mipango, mikakati, utekelezaji na mafanikio shughuli na mafanikio ya wizara,
  • Kuratibu taarifa kwa Vyombo vya Habari kuhusu Wizara na Taasisi zake;
  • Kusimamia shughuli za Mahusiano ya Umma na Huduma kwa Wateja
  • kushiriki katika mazungumzo, mijadala ya umma na vyombo vya habari juu ya masuala yanayohusu Wizara;
  •  Kuandaa na kutekeleza mikakati ya mawasiliano kwa Wizara;
  • Kutangaza shughuli za Wizara, programu na sera kupitia vyombo vya habari vya ndani na nje;
  • Kuratibu na kufanya maandalizi ya warsha, mikutano na makongamano ya Wizara;
  • Kusimamia na kuhuisha maudhui ya tovuti ya Wizara na ya serikali pamoja na mitandao mingine ya kijamii ya Wizara;
  • Kushirikiana mara kwa mara na Maafisa Habari katika taasisi zilizo chini ya wizara kwa ajili ya  kupata nyaraka na taarifa mbalimbali zinazohusu masuala ya elimu, mafunzo, sayansi, teknolojia na ubunifu kwa lengo la kutoa taarifa kwa ajili ya umma.