
Na
WyEST
DSM
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mzizima Maua Kibendu, ameishukuru Serikali kuwa kuwa kupitia Programu ya BOOST imewezesha ujenzi wa shule hiyo na kutoa mafunzo kwa Walimu 16, hali iliyochangia kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji kwa wanafunzi na kuibua vipaji vwa wanfunzi.
Wakizungumza kuhusu mafanikio ya programu hiyo wanafunzi Abiero Odwar na Subra Kumbata wote wanasoma darasa la sita wameeleza kuwa miundombinu bora na vifaa vya kutosha katika shule yao vinawawezesha kujifunza kwa weledi na kupata maarifa pamoja na kuwawezesha kuwa wabunifu.
Shule ya Msingi Mzizima imejengwa kwac gharama ya TZS. milioni 306.9 zilizotolewa na Mradi huo unaolenga Kuimarisha na Kuboresha Elimu ya Awali na Msingi Tanzania Bara (BOOST)