Wadau wa Elimu kutoka nchini Norway wamekutana na kuzungumza na Naibu Katibu Mkuu Dkt. Franklin Rwezimula juu ya ushirikiano wa masuala ya Elimu ya Juu, Utafiti na mabadiliko ya tabia nchi.
Dkt. Rwezimula amesema Watanzania wengi wanaendelea kunufaika na ushirikiano huu ikiwa ni pamoja na kupata ufadhili wa masomo ya Elimu ya Juu nchini Norway, pamoja na unanzishwaji wa miradi 18 na Taasisi 9 nchini kutoka kwenye programu ya NORHED.
Norway itaendelea kusaidia katika Utafiti na masomo Elimu ya juu nchini Tanzania pamoja na kuinua vitengo vya utafiti nchini na kuimarisha umoja baina ya Tanzania na Norway kwenye Elimu ya juu na Utafiti, hayo yamesemwa hii leo tarehe 26/6 na Dr. Grete Benjaminsen Mshauri Mkuu wa Sekta ya Utafiti na Elimu ya juu nchini Norway.
Ikumbukwe mnamo Septemba 2023 Serikali ya Tanzania iliingia makubaliano na Norway kuhusu masuala ya mabadiliko ya tabia nchi kwa lengo la kuimarisha sera za kupambana na mabadiliko ya tabia nchi ikiwa ni pamoja na uanzishwaji wa Programu za Utafiti, na mwezi Oktoba 2023 makubalino baina ya COSTECH na Norway yalisainiwa.