Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Taasisi ya Flaviana Matata Foundation leo, Agosti 7, 2025, wamekutana jijini Dodoma kujadili rasimu ya makubaliano ya ushirikiano wa kimkakati unaolenga kuimarisha sekta za elimu, afya na mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia kwa watoto wa kike nchini.


 Miongoni mwa maeneo yatakayowekewa mkazo ni pamoja na kuboresha miundombinu ya shule kwa kujenga na kukarabati vyoo, kuanzisha vyumba maalum kwa ajili ya wasichana kujisitiri wakati wa hedhi, pamoja na kujenga sehemu za kuchomea taka (incinerator).


Aidha, taasisi hiyo inalenga kutoa ufadhili wa masomo kwa wasichana ngazi ya sekondari mpaka Chuo kikuu wanaotoka katika mazingira magumu, kutoa elimu kuhusu afya ya uzazi, hedhi salama, na ukatili wa kijinsia, pamoja na kugawa taulo za kike na vifaa vya kujifunzia na kufundishia.

Ushirikiano huu unatarajiwa kuleta mabadiliko chanya katika maisha ya wasichana nchini, kwa kuboresha upatikanaji wa elimu na huduma bora za afya, sambamba na kuimarisha juhudi za Serikali katika kuleta usawa wa kijinsia na maendeleo endelevu.