Kamati ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo ikiongozwa na Mwenyekiti Mh. Husna Juma Sekiboko imeridhiswa na ujenzi wa Shule maalum ya wasichana ya Mkoa wa Dar es salaam.



Shule hii ni moja kati ya Shule 26 za Sekondari za wasichana za Sayansi zilizojengwa nchini ili kuongeza fursa za wanafunzi wa kike kusoma masomo ya Sayansi. Shule hizi zinajengwa kupitia Programu ya Uboreshaji wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP)



katika Mkoa wa Dar es Salaam kupitia SEQUIP pamoja na Shule hiyo maalum ya Wasichana shule nyingine tatu zimejengwa ikiwemo Shule ya Msakuzi Sekondari, Ubungo NHC na Shule ya Sekondari King'azi ili kusogeza huduma ya elimu za sekondari karibu na makazi hivyo kupunguza umbali wa wanafunzi kwenda na kurudi shule.



Ujenzi wa Shule zote nne kwa ujumla unatarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 5.8.



Shule ya Wasichana ya Mkoa wa Dar es Salaam mpaka sasa ina jumla ya wanafunzi 499 ambapo wanafunzi wa kidato cha kwanza ni 176, kidato cha tano 191 na kidato cha nne 133