Kamishna wa Elimu Dkt. Lyabwene Mtahabwa amesema Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023 inasisitiza suala la upatikanaji wa huduma bora ya chakula na lishe kwa Wanafunzi Shuleni ili kuwaepusha kukatiza masomo kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo njaa.
Dkt. Lyabwene amesema hayo leo Julai 25, 2024 jijini Dodoma katika Kongamano la Kitaifa la Utoaji Chakula na Lishe Shuleni, akisisiza kuwa kauli Mbiu ya Kongamano hilo inaakisi matakwa ya Sera ya Elimu na hivyo ni muhimu kuzingatia
"Ili waweze kujifunza vizuri, Wanafunzi wetu wanahitaji mazingira bora na salama pamoja na kuwa na afya bora ya kimwili na kiakili" alisema Kamishna huyo.
Kamishna huyo amewaeleza Wadau wa Kongamano hilo kuwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inatekeleza Mpango wa Shule Salama na kwamba katika Mpango huo suala la lishe Shuleni ni la muhimu na linazingatiwa.
Ni kweli Wizara inatoa Sera, nyaraka na miongozo mbalimbali kwa ajili ya utekelezaji wa afua za kielimu. Lakini utekelezaji wa nyaraka hizo muhimu unategemea sana ushiriki wa Wadau wote