
Dar es Salaam- Hafla ya kutangaza washindi wa Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu 2026 imefanyika katika ukumbi wa The Superdome, Masaki jijini Dar es Salaam, ikihudhuriwa na viongozi wa kitaifa na wadau wa fasihi. Washindi walikabidhiwa tuzo pamoja na mfano wa hundi za zawadi zao.

Katika kipengele cha riwaya, mshindi wa kwanza ni Bishop John Hiluka kupitia kazi yake Waraka kutoka Gerezani. Nafasi ya pili imechukuliwa na Halfani Sudi kwa Mnara wa Posta, huku nafasi ya tatu ikienda kwa Enock Maregesi kwa Alama za Bluu.

Kwa upande wa ushairi, mshindi wa kwanza ni Abdalaj Salum Ngereza kwa diwani ya Muwinda Elimu. Nafasi ya pili imechukuliwa na Kombo Abdalah Omar kwa Tunu ya Taifa, na nafasi ya tatu imeenda kwa Hafidh Makame kwa Naisubiria Faraja.

Katika kipengele cha hadithi za watoto, mshindi wa kwanza ni Amina Abdulrahman Mohamed kwa kazi yake Shumi na Vitungule, huku nafasi ya tatu ikinyakuliwa na Fatma Suleiman kwa Kidau cha Panya.

Kwa kipengele cha tamthilia, mshindi wa kwanza ni Hamis Kibari kwa Ufalme wa Mabadiliko, na nafasi ya tatu imechukuliwa na Esther Nyawale kupitia Jiko la Ukombozi.


