Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda Julai 30, 2024 ameweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Chuo cha Ufundi Arusha Kampasi ya Kikuletwa itakayokuwa Kituo cha Umahiri cha Nishati Jadidifu.



Kampasi hiyo inajengwa katika Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro ambapo ikikamilika itakuwa na uwezo wa kuzalisha wataalamu wa Nishati Jadidifu wasiopungua 1,500 kwa Mwaka.



Kituo hicho cha Umahiri kinajengwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Benki ya Dunia kupitia Mradi wa Kujenga Ujuzi na Kuimarisha Ushirikiano wa Kikanda wa Afrika Mashariki unagharimu zaidi ya Bilioni 36.