
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Aprili 13, 2025, nchini Saudi Arabia, imesaini Hati ya Makubaliano ya ushirikiano na Wizara ya Elimu ya Saudi Arabia katika kuendeleza Sayansi Sayansi Teknolojia na Elimu.
Hati hiyoo wa Makubaliano imesainiwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda na Mhe. Yousef bin Abdullah Al-Benyan, Waziri wa Elimu na Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya HCDP nchini Saudi Arabia,
Tukio hilo limeshuhudiwa na Katibu Mkuu, Prof. Carolyne Nombo, Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Dkt. Mohammed Juma Abdalla, Mkurugenzi wa Elimu ya Juu Prof. Peter Msofe na Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya ufundi Stadi Dkt. Fredrick Selukele.
Lengo kuu la makubaliano hayo ni kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizi mbili katika masuala ya elimu, utafiti, na sayansi