Wahariri wa Vyombo vya Habari walipitishwa katika utekelezaji wa Mitaala iliyoboreshwa ya Mwaka 2023 ili wawe na uelewa wa maboresho hayo



Wahariri walipitishwa katika utekelezaji huo Mechi 07, 2024 Jijini Dar ea Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu (TET) Dkt. Anneth Komba wakati wa Mkutano wao na Viongozi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia uliolenga kuzungumza na kujadili juu ya mageuzi makubwa katika sekta ya elimu.



Dkt. Komba aliwaeleza Wahariri hao kuwa utekelezaji wa Mitaala iliyoboreshwa ulianza tangu Januari 2024 ambapo kwa ngazi ya Sekondari Mitaala hiyo imeanza kwa wanafunzi wa Sekondari Mkondo wa Elimu ya Amali ambao watafanya mitiani ya NACTVET ya Umahiri



Aidha, Mkurugenzi Mkuu huyo ameongeza kuwa utekelezaji wa mitaala ya Elimu ya Sekondari ya Chini Mkondo wa Jumla utaanza Januari 2025 ambao una michepuo 11 na Mitaala ya Elimu ya Sekondari Hatua ya Juu itaanza kutekelezwa Julai 2024 kwa wanafunzi watakaoingia kidato cha Tano.