Serikali inaendelea kutoa fursa kwa Sekta Binafsi na Taasisi za Dini kuwekeza katika kujenga Vyuo Vikuu ili kuongeza nafasi za masomo ya elimu ya Juu na kupanua wigo wa programu za mafunzo kulingana na mahitaji ya Kitaifa na Kimataifa.
Tarehe 19 April Jijini Dar es Salaam Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amezindua Chuo Kikuu cha Tumaini Dar es Salaam (DarTU) kinachomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani.
Uzinduzi huo umeshuhudiwa na Viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Albert Chalamila wakiongozwa na Askofu Mkuu wa KKKT na Mkuu wa Chuo hicho Dkt. Alex Malasusa