Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema Septemba 16, 2023 Wizara itatangaza Washindi wa Tuzo za Watafiti Mahiri waliochapisha Matokeo ya tafiti zao katika Majarida yenye hadhi ya Juu Kimataifa (High Impact Factor Journals).

Prof. Mkenda ametoa kauli hiyo Septemba 11, 2023 jijini Dodoma wakati akizungumza na Kamati ya Tuzo hizo iliyowasilisha taarifa baada ya kukamilisha zoezi la uhakiki wa maombi ya tuzo hizo.

Kupitia kikao hicho mapendekezo mbalimbali yamejadiliwa kuhusu tuzo hizo zinazolenga kuhamasisha Watafiti wa ndani pamoja na kuimarisha uwezo wa Nchi katika kufanya tafiti ili kuchagiza Maendeleo kiuchumi.