Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Elimu) Atupele Mwambene amesema Ofisi ya Rais TAMISEMI itaendelea kusimamia zoezi la ubainishaji na kuhakikisha Watoto wenye mahitaji maalum wanaandikishwa shule na kupatiwa afua stahiki kulingana na mahitaji yao.
Mwambene ameeleza hayo Septemba 20, 2024 jijini Arusha, katika Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 30 ya Elimu Jumuishi, ambapo amesema pamoja na jukumu hili pia itaendelea kuimarisha vituo vya malezi kwa Wanafunzi wenye mahitaji Maalum.
"Ofisi ya TAMISEMI itatekeleza kwa vitendo kuhakikisha wanafunzi wenye mahitaji maalum wanajengewa maadili mazuri kwa kuimarisha vituo vya malezi, ushauri na unasihi ili viweze kutoa huduma bora" Alisema Mwambene.
Aidha amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kuwatumia walimu wa elimu maalum na wadau mbalimbali katika kukuza vipaji na vipawa vya wanafunzi wenye mahitaji maalum