Kaimu Katibu Mkuu Wizra y Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe amekabidhi Vishkwambi 6,000 kwa Baraza la Mitihani Tanzania NECTA

Makabidhiano hayo yamefanyika julai 20, Jijini Dodoma.

Mdoe amesema huu ni mwendelezo wa utekekezaji wa mpango wa ugawaji vishkwambi kwa walimu na wakufunzi nchini ambavyo vilinunuliwa na Serikali na kutumika kwa ajili ya Sensa na hatimae vigawiwe kwa walimu, wakufunzi, Wathibiti Ubora na Maafisa Elimu.

Mdoe amesema tayari vishkwambi vimeshatolewa kwa walimu, wakufunzi wa vyuo vya ualimu na vya Maendeleo ya Wananchi wote na sasa ni zamu ya Baraza ambap kwa sasa wanatekeleza majukumu yao kwa kiasi kikubwa kupitia mifumo ya kidigitali.

Mdoe amesisitiza juu ya umuhimu wa kuwapatia mafunzo watumidhi eote watakao pokea Vishkwambi hivyo kama ambayo sasa Mafunzo yanaendele kwa walimu, wakufunzi , Wathibiti Ubora na maafisa Elimu wote waliopokea vishkwambi kama alivyoagiza Rais wa Jamhuti ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza katika makabidhiano hayo Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa Tanzania (NECTA) Dkt. Said Mohamed ameishukuru serikali kwa kupata Vishkwambi hivyo ambapo amesema vinaenda moja kwa moja kusaidia utendaji kazi katika kupitia mifumo ukiwemo wa Usajili wa Watahiniwa na ule wa usahishaji Mitihani. Kidijitali ( _E-Marking_ )