Jumla ya Walimu Wakuu 20,661 wa shule za msingi za Serikali na Sizizo za serikali nchini wamepewa mafunzo kuhusu utekelezaji wa mitaala ya Elimu ya Awali na Msingi iliyoboreshwa mwaka 2023.



Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt. Aneth Komba amesema kuwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais-TAMISEMI kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania imekamilisha kazi ya utoaji wa mafunzo hayo yaliyoanza tarehe 5 Mei, 2024, na kuhitimishwa tarehe 12 Juni, 2024 katika mikoa 26 ya Tanzania Bara.