Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, leo Januari 15, 2025, jijini Dodoma, amekutana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene, pamoja na Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa.



Kikao hicho kimejadili juu ya ajira za walimu kwa kuzingatia matakwa ya utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023