Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limejiandaa kutekeleza mabadiliko yanayotokana na Sera Mpya ya elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 Toleo la 2023 na mabadiliko ya mitaala ya elimu, na kwamba rasimu ya awali ya maeneo yote ambavyo yanatakiwa kutekelezwa katika Sera hiyo tayari imeandaliwa.
Kauli hiyo imetolewa Novemba 30, 2023 jijini Dar es salaam na Katibu wa Baraza hilo Dkt. Said Mohamed wakati akizungumza katika Ufunguzi wa Maadhimisho ya Baraza la mitihani Tanzania (NECTA).