Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda tarehe 18,01,2024 amekutana na kufanya mazungumzo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Bi. Ruth Zaipuna alipomtembelea katika Ofisi za Wizara, Dodoma.
Viongozi hao wamejadili mikakati ya kuendeleza ushirikiano na ufadhili wa Benki katika Miradi mbalimbali ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ikiwemo Wiki ya Ubunifu, uimarishaji Shule za Sekondari za Ufundi na Uandishi Bunifu.