Katibu Mkuu Prof. Nombo ameongoza kikao kati ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia , NMB BANK, NMB Foundation walioambatana na mshirika wao kutoka Shirika la "Save the Children"
ambapo wajadiliana namna ya kushirukiana katika utekelezaji wa mipango ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
Kikao hiki kimefanyika Machi 22, 2024 Jijini Dodoma ambapo Mkurugenzi Mkuu wa NMB Foundation Nelson Karumuna ametambulisha programu iitwayo Nuru Yangu Scholarship inayojikita kwenye ufadhili katika eneo la Ufindi, Ufundi Stadi na Mafunzo ya Ufundi kwenye michepuo ya Uhandisi, TEHAMA,Famasia, Mafuta, Gesi na Udaktari.
Karumuna amesema kuwa NMB Foundation inalenga kusaidia vijana waliopo nje ya mfumo rasmi wa elimu na kwamba Shirika la Save the Children limetenga sh 300 milioni za Kitanzania ambazo zitatolewa kwa NMB foundation ili kuwezesha Jukumu lake la kuwezesha sekta ya elimu hususani makundi ambayo yapo kwenye mfumo usio rasmi wa elimu yani Out of school programu.