MAJUKUMU YA KITENGO ELIMU MAALUM
1. Kusimamia utayarishaji wa Sera, Kanuni, Miongozo kuhusu mahitaji maalum ya kielimu nchini.
2. Kusimamia kituo cha kitaifa cha huduma za kielimu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum
3. Kusimamia uandaaji mpango endelevu wa utafutaji wa rasimali kwa ajili ya kugharamia elimu kwa wenye mahitaji maalumu kuanzia ngazi ya Awali hadi Vyuo Vikuu.
4. Kusimamia maandalizi ya miongozo kuhusu kuendeleza vipaji na vipawa vya wanafunzi kunzia Elimu ya Awali mpaka Vyuo Vikuu.
5. Kusimamia utayarishaji na uchambuaji wa data zinazohusu wanafunzi wenye mahitaji maalumu kuanzia Awali hadi Vyuo Vikuu katika mfumo wa data na sekta ya elimu na katika mtandao wazi wa Serikali na wabia na wadau mbalimbali.
6. Kusimamia uendelezaji wa mikakati ya ushrikiano baina ya Serikali/Taasisi zinazotoa huduma kwa watu wenye ulemavu na za wenye ulemavu wenyewe.
7. Kusimamia uendeshaji wa tafiti za elimu kuhusu elimu maalumu na kuzishauri wamiliki kuhusu uendeshaji bora wa taasisi husika.
8. Kusimamia maandalizi ya viwango na mitaala inayohusu wanafunzi wenye mahitaji maalumu ya elimu
9. Kusimamia uanzishaji, uendelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa miradi na programu kuhusu elimu maalumu.
10. Kusimamia uandaaji na uwasilishaji taarifa za utekelezaji wa kazi kama itakavyotakiwa.
MIONGOZO
1. MWONGOZO WA KITAIFA WA UBAINISHAJI NA UPIMAJI WA WATOTO WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUMU YA KIELIMU
2. MWONGOZO WA ZIARA YA NYUMBANI KWA WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUMU
3. MWONGOZO WA SHULE YA NYUMBANI KWA WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUMU