IDARA  YA  ELIMU YA JUU

  • Lengo

Kuhakikisha ubora na maendeleo madhubuti ya sera za kisekta za elimu ya juu pamoja na uhamasishaji wa upatikanaji wa  rasilimali ili kuongeza upatikanaji na usawa wa elimu.

 

  • Majukumu/Kazi

Idara hii itafanya kazi zifuatazo:

i.   Kutoa maoni katika uundaji, ufuatiliaji, tathmini na mapitio ya utekelezaji wa sera ya elimu ya juu;

ii.  Kuanzisha, kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa mpango wa maendeleo wa elimu ya juu wa wizara pamoja na programu na miradi yake;

iii. Kuandaa miongozo na mikakati ya kutambua na kuendeleza vipaji katika elimu ya juu;

iv. Kuchochea maendeleo ya elimu ya juu kwa viwango vya kimataifa, ikiwemo kutoa ushauri juu ya uhusiano wa elimu ya juu na mahitaji ya maendeleo ya jamii;

v.  Kushirikiana na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) na taasisi nyingine za kitaalamu katika kuleta maendeleo bora yanayohusiana na ujuzi unaotokana na elimu ya juu nchini;

vi. Kushirikiana na Baraza la Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki na mashirika mengine ya kikanda ili kukuza na kudumisha ushirikiano wa kikanda na kimataifa katika elimu ya juu; na

vii. Kukuza uelewa kwa umma kuhusu kazi na majukumu ya idara  ya elimu ya juu.

Idara hii itaongozwa na Mkurugenzi na itakuwa na vitengo viwili kama ifuatavyo:

 

a.  Kitengo cha Uratibu wa Elimu ya Juu; na

b.  Kitengo cha Maendeleo ya Elimu ya juu

 

Kitengo cha Uratibu wa Elimu ya Juu

Kitengo hiki kitafanya shughuli zifuatazo:

i.  Kuchambua, kutafsiri, kuwezesha utekelezaji, kufuatilia, kutathmini na kutoa ushauri kuhusu utekelezaji wa sera ya Elimu na Mafunzo pamoja na mpango wa Taifa wa maendeleo ya Elimu ya juu.

ii.  Kutoa maoni katika uandaaji wa sera mbalimbali za elimu ya juu, ikiwamo masuala ya maendeleo ya ufadhili wa elimu hiyo.

iii. Kuchambua, kutafsiri na kuwezesha utekelezaji wa mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, itifaki zake na nyaraka nyingine za kikanda na kimataifa kuhusu elimu ya juu.

iv. Kuandaa au kusimamia maandalizi ya Kongamano la kila mwaka la Elimu ya Juu kwa kushirikiana na wadau wa taasisis za  elimu ya juu.

v.  Kuhamasisha umma kuhusu fursa za elimu ya juu, mifumo ya kugharamia elimu hiyo, marejesho ya mikopo, sera za uwekezaji, mikakati na mipango ya utekelezaji.

vi. Kuanzisha, kuendeleza na kuhamasisha upatikanaji wa rasilimali kwa ajili ya maendeleo ya elimu ya juu nchini.

vii. Kukuza programu za ushirikiano endelevu kati ya taasisi za mafunzo ya elimu ya juu, viwanda na biashara.

Kitengo hiki kitaongozwa na Mkurugenzi Msaidizi

 

Kitengo cha Maendeleo ya Elimu ya juu

Kitengo hiki kitafanya shughuli zifuatazo:

i.  Kusimamia na kuhamasisha maendeleo ya taasisi za elimu ya juu zilizo chini ya wizara;

ii.  Kuanzisha na kubuni taasisi mpya za elimu ya juu kwa kuzingatia mahitaji ya maarifa na ujuzi unaohitajika nchini;

iii.  Kuandaa miongozo na mikakati ya kutambua na kuendeleza vipaji katika elimu ya juu na kusimamia utekelezaji wake;

iv.  Kukuza na kusimamia upatikanaji, ubora na usawa katika elimu ya juu kwa gharama nafuu;

vii. Kuratibu masuala ya ushirikiano yanayohusu elimu ya juu;

viii. Kushauri, kuhamasisha, kuimarisha na kuwezesha upatikanaji wa ufadhili wa masomo wa ndani na nje ya nchi, mikopo na mahitaji kwa wanafunzi na wafanyakazi wa elimu ya juu;

ix.  Kusaidia na kuwezesha ukuaji wa ustawi wa wanafunzi na wafanyakazi wa taasisi za elimu ya juu;

x.   Kusimamia na kuhamasisha ustawi wa wanafunzi wa Tanzania wanaosoma nje ya nchi kwa kushirikiana na wizara zinazohusika na mambo ya nje na mahusiano ya kimataifa;

xi.   Kutunza na kuboresha taarifa za usajili wa ufadhili na udhamini wa wanafunzi wa ndani na nje ya nchi.

xii.  Kufanya ufuatiliaji wa wahitimu, kuandaa na kuboresha taarifa kuhusu ajira pamoja na ujuzi wao na kutoa ushauri kwa mamlaka za udhibiti na za kitaalamu.

xiii. Kushauri kuhusu vigezo, miongozo na taratibu za utoaji wa ufadhili wa masomo, pamoja na miradi na mikopo ya elimu ya juu;

xiv. Kusimamia upatikanaji wa vibali vya makazi kwa wahadhiri wa kigeni, wanafunzi na wanaojitolea.

Kitengo hiki kitaongozwa na Mkurugenzi Msaidizi

 

HEET PROJECT - ENVIRONMENTAL AND SOCIAL IMPACT ASSESSMENT REPORTS 

HEET PROJECT - APROVED ESIA REPORTS FROM WB