Idara ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu
Lengo
Kutoa sera na miongozo ya utafiti na maendeleo bunifu kwa nia ya kubadili jamii kuwa inayotumia maarifa.

Kazi
1. Kutunga na kupitia sera za sayansi, teknolojia, ubunifu na utafiti, miongozo, viwango na kufuatilia utekelezaji wake;
2. Kukuza ubunifu na matumizi ya sayansi na teknolojia nchini;
3. Kuweka mazingira wezeshi katika sayansi, teknolojia na ubunifu nchini;
4. Kuendeleza wataalamu wenye taaluma za sayansi na teknolojia kwa kushirikiana na Wizara/sekta husika;
5. Kuanzisha na kusimamia taasisi za sayansi na teknolojia nchini;
6. Kuandaa na kuratibu utendaji kazi wa Mfumo wa Kitaifa na Ubunifu;
7. Kuchochea tasnia na sekta binafsi kuongeza uwekezaji wake katika maendeleo ya Sayansi na Teknolojia na Ubunifu; na
8. Kuanzisha na kuendesha usimamizi wa Mfuko wa Taifa wa Utafiti.

Idara hii inaongozwa na Mkurugenzi na ina Sehemu mbili:
a) Utafiti na Maendeleo; na
b) Sayansi na Teknolojia.