Uwazi:  Watumishi wetu watakuwa wanatoa maelekezo ambayo ni wazi na yanayoeleweka wakati wa utoaji wa huduma katika eneo la elimu, sayansi, teknolojia na ubunifu

Uwajibikaji:  Wizara itawajibika katika maamuzi yanayohusiana na utoaji wa elimu, sayansi, teknolojia na ubuinifu;

Weledi:  Wizara itahakikisha uwepo wa watumishi wenye ujuzi, umahiri, maarifa na uelewa katika kutekeleza majukumu yake katika eneo la elimu, sayansi, teknolojia na ubunifu;

Uadilifu:  Tutazingatia misingi ya maadili ya Utumishi wa Umma katika kufikia malengo yetu;

Ubunifu:  Tutakuza ujuzi , umahiri, na uvumbuzi katika utoaji wa huduma za elimu na mafunzo ili kuleta mabadiliko chanya kupitia sayansi, teknolojia na ubunifu; na

Kufanya kazi kwa ushirikiano (Teamwork): Tutafanya kazi kwa kushirikiana na kuunganisha juhudi zetu ili kufikia malengo ya Wizara na kuchangia katika maendeleo ya Taifa.