1.0 Utangulizi

Sehemu ya Elimu ya Ualimu inahusika na uratibu, usimamizi na maendeleo ya Elimu ya Ualimu nchini. Kupitia utekelezaj wa Sera, Sheria, Kanuni, Taratibu, na Miongozo, Sehemu hii ina jukumu la kuandaa walimu wa shule za Awali na Msingi wenye sifa stahiki, mahiri, weledi wa kitaalamu na kitaaluma pamoja na maadili ili kuboresha ubora wa elimu. Aidha, ina jukumu la kuimarisha maandalizi na maendeleo endelevu ya walimu kulingana na mahitaji ya mfumo wa elimu. 

Sehemu hii iko chini ya Idara ya Elimu Msingi katika ofisi ya kamishna wa Elimu. Aidha, sehemu hii inaongozwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Elimu ya Ualimu.

1.1 Majukumu ya Sehemu ya Elimu ya Ualimu:Sehemu hii  inashughulikia majukumu yafuatayo:

  1. i.  Kuratibu utekelezaji, kufuatilia, kufanya tathmini na kutoa ushauri kuhusu utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo pamoja na nyenzo zake katika elimu ya awali, msingi, sekondari, elimu maalum na mafunzo ya ualimu.
  2. ii.  Kutoa mchango wa kitaalamu katika uandaaji wa sera na nyenzo mbalimbali za elimu zinazohusu elimu ya awali, msingi, sekondari pamoja na elimu maalum na elimu ya watu wazima kwa walimu.
  3. iii. Kuandaa miongozo na mikakati ya kubaini na kuendeleza vipaji katika vyuo vya ualimu na kuhakikisha utekelezaji wake.
  4. iv. Kuandaa na kuwasilisha taarifa za m.nm . maendeleo kuhusu elimu ya ualimu kwa walimu wa elimu ya awali, sekondari na elimu maalum ili kusaidia michakato ya uundaji na uboreshaji wa sera.
  5. v. Kuanzisha, kuendeleza, kuweka au kuhamasisha programu za maendeleo endelevu ya kitaaluma kwa wakufunzi pamoja na kuimarisha ushirikiano kati ya sekta ndogo ya mafunzo ya ualimu, viwanda na biashara.

1.2 Huduma Zinazotolewa na Sehemu ya Mafunzo ya Elimu ya Ualimu:

  • Udahili wa wanachuo katika Vyuo vya Ualimu
  • Uendeshaji wa Vyuo vya Ualimu vya Serikali
  • Usimamizi wa Elimu ya Ualimu nchini

VYUO VYA UALIMU VYA SERIKALI

AINA YA MAFUNZO YA UALIMU NA VYUO VINAVYOTOA MAFUNZO HAYO

MFUMO WA UDAHILI ELIMU YA UALIMU (TCMS)