Afisa Elimu Mkoa wa Tabora Mwl. Upendo Rweyemamu amesema Serikali Mkoani humo inaendelea kutekeleza program za elimu ya Watu Wazima kuhakikisha inatoa fursa ya elimu kwa wote.



Akizungumza katika Kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya Juma la Elimu ya Watu Wazima Upendo amesema Mkoa huo umefanikiwa kutekeleza program ya Mpango wa Elimu Changamani kwa Vijana walio nje ya Shule (IPOSA) ambayo mpaka sasa ina vituo 40 vyenye Wanafunzi 1,041.



Ameongeza kuwa program ya Mpango wa Elimu Msingi kwa Walioikosa (MEMKWA) ina vituo 100 ikiwa na Wanafunzi 4,204.



Aidha Mwl. Upendo ameongeza kuwa pamoja na mafanikio hayo bado kuna changamoto kubwa ya Wanafunzi kutoandikishwa Shule.



"Mwaka 2024/25 Mkoa wa Tabora umesajili Wanafunzi wa Elimu ya Awali asilimia 60 pekee" Alisema Upendo