Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Michezo na Utamaduni Mhe. Husna Sekiboko amesema bunifu katika Maoesho ya mwaka huu zimejikita katika kutatua changamoto zilizopo katika jamii.
Mhe. Sekiboko amesema hayo Mei 31, 2024, jijini Tanga wakati akizungumza katika Kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu.
"Kama Bunge tunajivunia kazi nzuri zilizofanywa katika Maonesho haya, sisi tunapongeza juhudi za serikali katika kuboresha bunifu Nchini" amesema Sekiboko.
Mhe. Sekiboko ameitaka Wizara Elimu, Sayansi na Teknolojia kutoa elimu kuhusu Sera ya Elimu na Mitaala iliyoboreshwa ili Wazazi na Walezi wapate uelewa wa kutosha kuhamasisha watoto wao kusoma Elimu ya Amali.