Katibu Mkuu wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amesema bado kuna uhitaji mkubwa wa kuhamasisha jamii na wadau mbalimbali kushiriki kikamilifu katika kuhamasisha na kuchangia uwepo wa huduma ya chakula na lishe katika shule za Awali, Msingi na Sekondari.



Prof. Nombo ameeleza hayo Julai 26, 2024 wakati akizungumza katika Kongamano la Kitaifa la Utoaji wa Chakula na Lishe Shuleni akisisitiza kuwa uwepo wa huduma ya chakula na lishe shuleni inachagiza tendo la ujifunzaji na ufundishaji kufanyika kwa ufanisi.



Akitoa taarifa kuhusu Kongamano hilo, amesema wataalam kutoka Wizara za kisekta Mashirika mbalimbali na Vyuo Vikuu wameshiriki katika kujadili mada mbalimbali ikiwa ni pamoja na Uendelezaji wa Programu ya chakula shuleni, Huduma za afya na lishe shuleni pamoja matumizi ya vyakula vilivyorutubishwa na Upatikanaji wa taarifa za utoaji wa huduma ya chakula shuleni.