Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolokia Prof. Adolf Mkenda amesema Rombo inajivunia Maendeleo Makubwa katika Sekta ya Elimu



Akizungumza Disemba 23, 2024 wakati wa Rombo Marathon amesema kuwa wakati nchi inapata uhuru Rombo haikuwa na shule ya Sekondari lakini kwa sasa ina shule za sekondari 41.



Ameongeza kuwa Serikalinya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea na ujenzi wa Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA)