Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), inaendelea kuwekeza katika miundombinu mipya katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Mkwawa (MuCE).



Ujenzi wa miundombinu hiyo mipya unalenga kuongeza nafasi za udahili wa wanafunzi na kuboresha mazingira ya kujifunzia.



Miundombinu hiyo ni pamoja na jengo la  Multimedia na mahitaji maalum pamoja na jengo la sayansi, ambayo yatahusisha madarasa yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 400 na maabara zitakazokuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 950 hadi 1000 kwa wakati mmoja.



Majengo mengine ni ya hosteli za wanafunzi zitakayokuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 152, jengo jipya la maabara za Fizikia litakalokuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 120 na madarasa yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 240.



Miradi yote ya ujenzi imegharimu takribani shilingi bilioni 14. Uwekezaji huu utachangia moja kwa moja maendeleo ya kitaaluma na kiuchumi.