Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeazimia kuwa na Mfumo shirikishi wa kuandaa, kuratibu na kuchambua tafiti za kielimu kwa lengo la kuwezesha matokeo ya tafiti zinazofanyika kuwa na tija katika kuendelea kuimarisha Sekta ya Elimu nchini kwa wadau wote.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda jijini Dodoma alipokutana na Kamati ya wataalamu aliyounda yenye jukumu la kupitia mifumo iliyopo na kuandaa mapendekezo ya uboreshaji.



Kamati hiyo inahusisha wajumbe kutoka Wizara ya Elimu, Taasisi za utafiti, Taasisi za Elimu ya Juu na Wadau wa Maendeleo.



Katika hatua ingine Mkenda amesema Wizara inakwenda kuanza kutoka ripoti ya Mwaka ya Takwimu za Elimu ( Basic Education Statistics Tanzania ) inayohusisha taarifa za ngazi zote za Elimu na takwimu za shule na Vyuo Binafsi.