Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi watakiwa kuwa wabunifu katika kuangalia fursa zilizopo ili kuhakikisha wanazalisha wahitimu walio bora.
Wito huo umetolewa Oktoba 26, 2023 jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo wakati wa kikao chake na baadhi ya Wakuu wa Vyuo hivyo.
Prof. Nombo ameongeza kuwa mwelekeo wa Serikali ni kuzifanya taasisi zake zijitegemee badala ya kusubiri mafungu ya serikali pekee hivyo amewataka wakuu hao kuona namna ambavyo wataweza kutumia vifaa na nguvu kazi waliyonayo kwa ajili ya kuanza kujitegemea.
Aidha, Prof. Nombo amewataka Wakuu hao kufuata sheria, taratibu na miongozo inayotolewa na serikali katika kutekeleza majukumu yao.