
Mwalimu Komba wa Shule ya Sekondari Iyunga amesema kuwa Shule zilizopokea Vifaa vya Kidigitali vya kufundishia na kujifunzia watasimamia matumizi sahihi ya vifaa hivyo ili kuboresha elimu na ujuzi kwa vijana.

Akizungumza wakati wa ugawaji wa vifaa hivyo, kwa niaba ya shule zilizopokea vifaa Mwalimu Komba ameishukuru Serikali Kwa kuwapatia Vifaa hivyo vitakavyosaidia kwenye ufundishaji na ujifinzaji.

Ameeleza kuwa dhamira ya walimu ni hakikisha vifaa hivyo vinatumika kwa ufanisi ili kutoa matokeo bora.

"Tutahakikisha tunasimamia Vifaa kwa ufanisi na kuvitumia Kwa malengo yaliyokusudiwa," amesisitiza Mwl Komba


