Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda leo Januari 24,2024 ameungana na viongozi mbalimbali kushiriki kikao kati ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango na Makamu wa Rais wa Cuba, Mhe. Salvador Mesa, Ikulu Jijini Dar es Salaam.



Aidha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Cuba zimekubaliana kuimarisha ushirikiano wa maendeleo katika sekta za kipaumbele ambazo ni elimu, afya, kilimo na utalii.



Awali viongozi hao walishuhudia utiaji saini Hati za Makubaliano ya Ushirikiano (MoU) ikiwemo makubaliano kati ya Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) na Chuo Kikuu cha Artimesa Diaz Gonzalez cha Cuba.