Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda leo hii Novemba 05, 2024 Jijini Dodoma amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa COSTECH Dr Amos Nungu na kujadili juu ya maandalizi ya Kongamano la tisa la Kitaifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (STICE).



Kongamano hilo ambalo linajumuisha maonesho hufanyika kila mwaka likiwa na lengo la kuwakutanisha wanasayansi, Wabunifu, watunga Sera na wadau wote wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (STU) kujadili maendeleo ya STU.



Fuatilia mazungumzo ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda na vyombo vya habari hapo kesho tarehe 6 Novemba, 2024 kwa taarifa zaidi