Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo Julai 24,2024 Jijini Dodoma amekutana na Mkuu wa kitengo cha Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (UNICEF) Bw. Daniel Baheta na kufanya mazungumzo yanayolenga kuimarisha uhusiano katika sekta ya elimu.



Prof. Nombo amempongeza Bw. Baheta kwa kushirikiana na Wizara katika kutekeleza miradi na mipango mbalimbali ya sekta ya elimu na kuhakikisha hatua zaidi zinasonga mbele.



Prof. Nombo amemkabidhi Kiongozi huyo zawadi ya mwanasesere anayebeba dhana kubwa kulingana na utamaduni wa Kitanzania na Afrika kwa ujumla, ikiwa ni ishara ya shukrani na mshikamano aliouonesha Bw. Bahite katika kipindi chote alichohudumu Nchini, anayetarajia kuondoka nchini, kabla ya kupata uhamisho wa kikazi kuelekea nchini Sudani.



"Tutakukumbuka sana, kwani tumeshirikiana vyema ndani ya Sekta ya Elimu na umekua mwanafamilia ndani ya Wizara ye Elimu, Sayansi na Teknolojia" alisema Prof. Nombo.



Kwa nafasi yake Bw. Baheta ameshukuru kwa ushirikiano alioupata nchini Tanzania na kufurahi zaidi kuwa miongoni mwa familia ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, na ameahidi kuendelea kushirikiana katika kila nyanja za maendeleo ikiwemo zinazogusa sekta ya elimu nchini Tanzania.