Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Daniel Mushi Januari 11, 2025 amekagua ujenzi wa miundombinu mbalimbali katika Chuo Kikuu cha Elimu Mkwawa (MUCE) inayotekelezwa kupitia mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET).
Majengo yaliyokaguliwa ni pamoja na Jengo la Sayansi, Jengo la Multimedia na Elimu Maalum, jengo la Maabara ya Fizikia, maktaba na hosteli ambapo ujenzi umefikia asilimia 12.
Prof. Mushi amewasisitiza wakandarasi kununua vifaa mbalimbali vya ujenzi kutoka viwanda vya ndani kwa lengo la kuchangia ukuaji wa uchumi wa taifa na kutumia zana za usalama wakati wote wa kazi ili kuzuia ajali.
Pia amewahimiza makarani wa kazi kuhakikisha wanakuwepo kwenye maeneo ya ujenzi kwa ajili ya kusimamia na kufuatilia hatua zote za utekelezaji wa miradi.
Kwa upande wake, Rasi wa Chuo Kikuu cha Elimu cha Mkwawa (MUCE), Prof. Deusdedit Rwehumbiza, amemshukuru Naibu Katibu Mkuu huyo kwa ziara yake na kuahidi kutekeleza maagizo yote yaliyotelewa.
Ameahidi kuongeza ufanisi katika kusimamia miradi ya ujenzi ili kufanikisha malengo yaliyowekwa