Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo tarehe 14 Disemba 2025, amefanya ziara ya kikazi katika Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) mkoani Kagera, ambapo amekagua na kujionea utekelezaji wa mafunzo ya ufundi stadi yanayotolewa chuoni hapo.



Katika ziara hiyo, Prof. Nombo amepata fursa ya kutembelea karakana mbalimbali na kujionea kwa karibu utolewaji wa mafunzo kwa wanafunzi, pamoja na kuzungumza na wakufunzi kuhusu hali ya mafunzo, miundombinu na mahitaji ya chuo.



Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inaendelea kusimamia na kuimarisha mafunzo ya ufundi stadi nchini ili kuhakikisha yanakidhi mahitaji ya soko la ajira na maendeleo ya taifa.