Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Daniel Mushi amesema vyombo vya Habari vina mchango mkubwa katika maendeleo ya Taifa kiuchumi, hivyo ni muhimu wadau katika tasnia hiyo kufanya kazi kwa weledi.
Prof. Mushi amesema hayo Agosti 28, 2024 jijini Dar es Salaam wakati akimwakilisha Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda kufungua Mkutano wa Jumuiya ya Mawasiliano Afrika Mashariki (EACA) unaolenga kujadiliana namna ya kushughulikia changamoto na kutumia fursa zilizopo katika sekta ya habari na mawasiliano.
‘’Mkutano huu umekuja wakati muafaka tunapotarajia kuharakisha maendeleo ya kiuchumi ya nchi zetu kupitia njia za ubunifu na shirikishi za habari na mawasiliano’’ Alisema Prof. Mushi.
Amesisitiza kuwa jamii isiyo na uelewa wa kutosha juu ya taarifa zinazotolewa na vyombo vya Habari ikiwemo mitandao, inaweza kuangukia kwenye mtego wa habari potofu