Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo Oktoba 23, 2023 jijini Dar es Salaam alikutana na kufanya mazungumzo na Menejimenti ya Mtandao wa Elimu Tanzania ikiongozwa na Mratibu wa Mtandao huo Ochola Wayoga.\
Mazungumzo hayo yalilenga kuweka mipango shirikishi ya Kongamano la Kimataifa la Elimu ( IQEC ) la 2023 ambalo linatarajiwa kufanyika Novemba 27 – 29, 2023 jijini Dar es Salaam na kubeba kauli mbiu "Kutafakari upya Elimu katika Mapinduzi ya Nne ya Viwanda”
Katika kongamano hilo mambo mbalimbali yatajadiliwa ikiwemo utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 toleo la 2023 na ufadhili endelevu wa elimu nchini.