Mafunzo ya Mtaala ulioboreshwa kwa walimu wakuu 57 wa shule za msingi za Serikali na zisizo za Serikali yanaendelea katika Mkoani Kilimanjaro lengo ni kuongeza ufanisi katika usimamiaji wa utekelezaji wa Mtaala huo nchini.
Mafunzo hayo ya siku mbili yameanza Juni 11, 2024 ambapo yanaendeshwa na Waratibu kutoka Taasisi ya Elimu Tanzania kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja pamoja pamoja na OR TAMISEMI.
Mafunzo hayo yanaendelea katika vituo mbalimbali nchi nzima ambapo walimu wanapata fursa ya kufahamu Mtaala huo kiundani na mbinu mbalimbali za kuutekeleza ili ulete tija kwa taifa.