
Tanzania kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inatekekeza mradi wa GPE-TSP unaolenga.kuboresha mazingira ya walimu, kutoa mafunzo endelevu kazini kwa walimu pamoja na usimamizi bora wa elimu una thamani ya Sh. Bilioni 226.54.
Leo tarehe 4, Machi, 2025 wataalamu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Rais TAMISEMI wamekutana kuandaa nyaraka kwa ajili ufadhili wa nyongeza katika mradi huo. Uboreshaji wa Nyaraka hizo unalenga kujumuisha masuala ya ujumuishaji wa kijinsia katikankrdi ili kuhakikisha sera na mipango ya utekelezaji wa mradi yanazingatia usawa kwa walimu wa jinsia zote na mazingira jumuishi kwa wanafunzi wa makundi yote.