Naibu katibu Mkuu, Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia anaeshughulikia na elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe amewasili katika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya ziara ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof Adolf Mkenda kukagua miradi ya maendeleo katika Chuo hicho.