Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amekutana na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania Prof. Najat Mohammed aliyeteuliwa hivi karibuni na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prof. Najat Mohammed amefika Ofisi kwa Waziri Jijini Dodoma, 11.07.2024 kwa ajili ya kujitambulisha. TAEC ipo chini ya Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia yenye jukumu la kudhibiti na kuhamasisha matumizi ya mionzi na teknolojia ya nyuklia.