
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo leo Machi 13, 2026 imeanza ziara kukagua miradi ya elimu kwa lengo la kuhakikisha kunakuwa na ufanisi katika matumizi ya rasilimali za umma.

Kamati hiyo ikiwa mkoani Tanga, inatembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa kampasi mpya ya Chuo Kikuu Mzumbe.

Utekelezaji wa Mradi huu ni kielelezo cha dhamira ya Serikali kusogeza huduma za elimu ya juu karibu na wananchi na kukuza uchumi wa kanda ya kaskazini-mashariki.


